Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 32:10 - Swahili Revised Union Version

10 mimi sistahili hata kidogo hizo rehema zote na kweli yote uliyomfanyia mtumwa wako; maana nilivuka mto huo wa Yordani na fimbo yangu tu, na sasa nimekuwa makundi mawili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 sistahili hata kidogo fadhili ulizonipa kwa uaminifu mimi mtumishi wako. Nilipovuka mto Yordani, sikuwa na kitu ila fimbo; lakini sasa ninayo makundi haya mawili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 sistahili hata kidogo fadhili ulizonipa kwa uaminifu mimi mtumishi wako. Nilipovuka mto Yordani, sikuwa na kitu ila fimbo; lakini sasa ninayo makundi haya mawili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 sistahili hata kidogo fadhili ulizonipa kwa uaminifu mimi mtumishi wako. Nilipovuka mto Yordani, sikuwa na kitu ila fimbo; lakini sasa ninayo makundi haya mawili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Sistahili fadhili na uaminifu wako wote ulionitendea mimi, mtumishi wako. Nilikuwa na fimbo tu mkononi mwangu nilipovuka mto huu wa Yordani, lakini sasa nimekuwa makundi mawili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 mimi sistahili fadhili na uaminifu wako wote ulionitendea mimi mtumishi wako. Nilikuwa na fimbo tu mkononi mwangu nilipovuka mto huu wa Yordani, lakini sasa ninayo makundi mawili.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 mimi sistahili hata kidogo hizo rehema zote na kweli yote uliyomfanyia mtumwa wako; maana nilivuka mto huo wa Yordani na fimbo yangu tu, na sasa nimekuwa makundi mawili.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 32:10
33 Marejeleo ya Msalaba  

Abrahamu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu.


Naye akasema, Ee BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, nakuomba mambo yangu uyajalie yawe heri leo, ukamfadhili bwana wangu Abrahamu.


Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. BWANA akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu.


Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Abrahamu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii unayolala nitakupa wewe na uzao wako.


Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.


Kwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi, na vijakazi, na watumwa, na ngamia, na punda.


BWANA akamwambia Yakobo, Urudi katika nchi ya baba zako na kwa jamaa zako, nami nitakuwa pamoja nawe.


nami nina ng'ombe, na punda, na kondoo, na watumwa, na vijakazi; nami nimepeleka watu nimpashe bwana wangu habari, nipate neema machoni pako.


Ndipo Yakobo akaogopa sana, na kufadhaika sana, akawagawanya watu waliokuwa pamoja naye, na kondoo, na ng'ombe, na ngamia, wawe makundi mawili.


Basi Daudi akaja Mahanaimu. Naye Absalomu akauvuka Yordani yeye na watu wote wa Israeli pamoja naye.


Ndipo Daudi, mfalme, akaingia, akaketi mbele za BWANA, akasema, Mimi ni nani, Bwana MUNGU, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hadi hapa?


Lakini mwenye haki ataishika njia yake, Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu.


Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.


Nimemwambia BWANA, Ndiwe BWANA wangu; Sina wema ila utokao kwako.


Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kulia umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza.


Atakaa mbele za Mungu milele, Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi.


Umemfanya mdogo kuliko Mungu; Umemvika taji la utukufu na heshima;


Huendelea toka nguvu hata nguvu, Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu.


Fadhili na kweli zitakutana, Haki na amani zitakumbatiana.


Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing'aayo, Ikizidi kung'aa hata mchana mkamilifu.


Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.


Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake.


Wewe utamtimilizia Yakobo kweli yako, na Abrahamu rehema zako, ulizowaapia baba zetu tangu siku za kale.


Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.


Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini mbele ya Yesu, akisema, Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana.


Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu kwa lolote, nijapokuwa si kitu.


Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.


Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo