Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 32:11 - Swahili Revised Union Version

11 Uniokoe sasa kutoka kwa mkono wa ndugu yangu, mkono wa Esau, maana mimi ninamwogopa, asije akaniua, na kina mama pamoja na watoto.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Nakuomba uniokoe sasa kutoka kwa ndugu yangu Esau, maana nina hofu kuwa atatushambulia na kutuua sote, akina mama pamoja na watoto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Nakuomba uniokoe sasa kutoka kwa ndugu yangu Esau, maana nina hofu kuwa atatushambulia na kutuua sote, akina mama pamoja na watoto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Nakuomba uniokoe sasa kutoka kwa ndugu yangu Esau, maana nina hofu kuwa atatushambulia na kutuua sote, akina mama pamoja na watoto.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Nakuomba uniokoe kutoka kwa mkono wa ndugu yangu Esau, kwa maana ninaogopa kuwa atakuja kunishambulia, pia kina mama pamoja na watoto wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Nakuomba, uniokoe na mkono wa ndugu yangu Esau, kwa maana ninaogopa kuwa atakuja kunishambulia, pia mama pamoja na watoto wao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Uniokoe sasa na mkonowa ndugu yangu, mkono wa Esau, maana mimi ninamwogopa, asije akaniua, na kina mama pamoja na watoto.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 32:11
21 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. BWANA akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu.


Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ile baraka babaye aliyombariki. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.


Rebeka akaarifiwa maneno ya Esau, mwanawe mkubwa. Akatuma mtu kumwita Yakobo, mwanawe mdogo, akamwambia, Tazama, katika habari zake Esau, ndugu yako, anajifariji moyo wake, maana anakusudia kukuua.


Basi, Yakobo akapeleka wajumbe mbele yake kwenda kwa Esau nduguye mpaka nchi ya Seiri katika nyika ya Edomu.


Ndipo Yakobo akaogopa sana, na kufadhaika sana, akawagawanya watu waliokuwa pamoja naye, na kondoo, na ng'ombe, na ngamia, wawe makundi mawili.


Esau akaja mbio kumlaki, akamkumbatia, na kumwangukia shingoni, akambusu; nao wakalia.


Ndipo Daudi, mfalme, akaingia, akaketi mbele za BWANA, akasema, Mimi ni nani, Bwana MUNGU, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hadi hapa?


Unikomboe kutoka kwa dhuluma ya mwanadamu, Nipate kuyashika mausia yako.


Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana. Uniponye kutoka kwa wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.


Mungu, unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe.


Unilinde nafsi yangu na kuniokoa, Usiniache niaibike, maana nakukimbilia Wewe.


Unitegee sikio lako, uniokoe hima. Uwe kwangu mwamba wa nguvu, Ngome thabiti ya kuniokoa.


Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki, Uniokoe kutoka kwa mtu wa hila asiye haki.


Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuliko mji wa nguvu; Na mashindano ni kama mapingo ya ngome.


Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuri liwakalo moto; naye atatuokoa mkononi mwako, Ee mfalme.


Kwa sababu hiyo fitina itatokea kati ya watu wako, na ngome zako zote zitaharibiwa, kama vile Shalmani alivyoharibu Betharbeli, katika siku ya vita; mama akavunjikavunjika pamoja na watoto wake.


Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]


Kiota cha ndege kikitukia kuwa mbele yako njiani, katika mti wowote, au chini, chenye makinda au mayai, naye koo ameatamia juu ya makinda, au juu ya mayai, usimtwae yule koo pamoja na makinda;


Nao wakamlilia BWANA, wakasema, Tumefanya dhambi, kwa kuwa tumemwacha BWANA, na kuwatumikia Mabaali na Maashtorethi; lakini sasa tuokoe kutoka kwa mikono ya adui zetu, nasi tutakutumikia wewe.


Basi BWANA atuamue, akatuhukumu mimi na wewe, akaone, akanitetee neno langu, akaniokoe kutokana na mkono wako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo