Mika 7:13 - Swahili Revised Union Version Hata hivyo nchi itakuwa ukiwa kwa sababu ya hao wakaao ndani yake, kwa sababu ya matunda ya matendo yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini nchi yote nyingine itakuwa jangwa, kwa sababu ya uovu wa wakazi wake. Biblia Habari Njema - BHND Lakini nchi yote nyingine itakuwa jangwa, kwa sababu ya uovu wa wakazi wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini nchi yote nyingine itakuwa jangwa, kwa sababu ya uovu wa wakazi wake. Neno: Bibilia Takatifu Dunia itakuwa ukiwa kwa sababu ya wakazi wake, kwa sababu ya matunda ya matendo yao. Neno: Maandiko Matakatifu Dunia itakuwa ukiwa kwa sababu ya wakazi wake, kwa sababu ya matunda ya matendo yao. BIBLIA KISWAHILI Hata hivyo nchi itakuwa ukiwa kwa sababu ya hao wakaao ndani yake, kwa sababu ya matunda ya matendo yao. |
Katika siku hiyo miji yake yenye maboma itakuwa kama mahali palipoachwa ndani ya mwitu, na juu ya kilele cha mlima, palipoachwa mbele ya wana wa Israeli; napo patakuwa ganjo.
Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.
Nami nitawaadhibu kwa kadiri ya matendo yenu, asema BWANA; nami nitawasha moto katika msitu wake, nao utateketeza vitu vyote viuzungukavyo.
Na nchi hii yote pia itakuwa ukiwa, na kitu cha kushangaza; nayo mataifa haya yatamtumikia mfalme wa Babeli miaka sabini.
mkuu wa mashauri, muweza katika kutenda; ambaye macho yake yamefumbuka juu ya njia zote za wanadamu, kumpa kila mtu kwa kadiri ya njia zake, na kwa kadiri ya matunda ya matendo yake,
ukawaambie watu wa nchi, Bwana MUNGU asema hivi, kuhusu habari zao wakaao Yerusalemu, na katika nchi ya Israeli; Watakula chakula chao kwa kukitunza sana, na maji yao watayanywa kwa ushangao, nchi yao iwe ukiwa, kwa kukosa vitu vyote viijazavyo, kwa sababu ya udhalimu wao wote wakaao ndani yake.
Nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa na ajabu, na kiburi cha uwezo wake kitakoma; nayo milima ya Israeli itakuwa ukiwa, asipite mtu.
Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.
Ndipo watakapomwomba BWANA, asiwaitikie; naam, atawaficha uso wake wakati huo, kwa kadiri walivyotenda mabaya kwa matendo yao.
Kwa sababu hiyo atawatoa, hata wakati wa kuzaa kwake aliye na uchungu; ndipo hayo mabaki ya nduguze watawarudia wana wa Israeli.
Basi, kwa ajili ya hayo, mimi nami nimekupiga kwa pigo liumizalo sana; nimekufanya kuwa ukiwa, kwa sababu ya dhambi zako.