Mika 1:12 - Swahili Revised Union Version Maana wakazi wa Marothi wanasubiri kwa hamu kupata mema; Lakini maangamizi yameshuka toka kwa BWANA, Yamefika katika lango la Yerusalemu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakazi wa Marothi wanangojea msaada kwa hamu kubwa, lakini maangamizi yaja kutoka kwa Mwenyezi-Mungu karibu kabisa na lango la Yerusalemu. Biblia Habari Njema - BHND Wakazi wa Marothi wanangojea msaada kwa hamu kubwa, lakini maangamizi yaja kutoka kwa Mwenyezi-Mungu karibu kabisa na lango la Yerusalemu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakazi wa Marothi wanangojea msaada kwa hamu kubwa, lakini maangamizi yaja kutoka kwa Mwenyezi-Mungu karibu kabisa na lango la Yerusalemu. Neno: Bibilia Takatifu Wale wanaoishi Marothi wanagaagaa kwa maumivu wakingoja msaada, kwa sababu maangamizi yamekuja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hata katika lango la Yerusalemu. Neno: Maandiko Matakatifu Wale waishio Marothi wanagaagaa kwa maumivu wakingoja msaada, kwa sababu maangamizi yamekuja kutoka kwa bwana, hata katika lango la Yerusalemu. BIBLIA KISWAHILI Maana wakazi wa Marothi wanasubiri kwa hamu kupata mema; Lakini maangamizi yameshuka toka kwa BWANA, Yamefika katika lango la Yerusalemu. |
Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote.
Je! Umemkataa Yuda kabisa? Roho yako imeichukia Sayuni? Mbona umetupiga, tusiwe na dawa ya kutuponya? Tulitazamia amani, lakini hayakuja mema yoyote, tulitazamia wakati wa kupona, na tazama, kufadhaika tu!
Tulitazamia amani, lakini hayakuja mema yoyote; tulitazamia wakati wa kupona, na tazama, kufadhaika tu!
Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta BWANA?
Kwa maana majeraha yake hayaponyeki; Maana msiba umeijia hata Yuda, Unalifikia lango la watu wangu, Naam, hata Yerusalemu.
Akawaambia, Msiniite Naomi, niiteni Mara kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana.
Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia, akingojea; maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule mtu alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia.