Msiyahubiri mambo haya katika Gathi, Msiyatangaze katika njia za Ashkeloni; Wasije wakashangilia binti za Wafilisti, Binti za wasiotahiriwa wakasimanga.
Mika 1:10 - Swahili Revised Union Version Msiyahubiri haya katika Gathi, msilie kamwe; Katika Beth-le-Afra ugaegae mavumbini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Msiitangaze habari hii huko Gathi, wala msilie machozi! Huko Beth-leafra mgaegae mavumbini kwa huzuni. Biblia Habari Njema - BHND Msiitangaze habari hii huko Gathi, wala msilie machozi! Huko Beth-leafra mgaegae mavumbini kwa huzuni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Msiitangaze habari hii huko Gathi, wala msilie machozi! Huko Beth-leafra mgaegae mavumbini kwa huzuni. Neno: Bibilia Takatifu Usiliseme hili huko Gathi; usilie hata kidogo. Huko Beth-le-Afra gaagaa mavumbini. Neno: Maandiko Matakatifu Usiliseme hili huko Gathi; usilie hata kidogo. Huko Beth-le-Afra gaagaa mavumbini. BIBLIA KISWAHILI Msiyahubiri haya katika Gathi, msilie kamwe; Katika Beth-le-Afra ugaegae mavumbini. |
Msiyahubiri mambo haya katika Gathi, Msiyatangaze katika njia za Ashkeloni; Wasije wakashangilia binti za Wafilisti, Binti za wasiotahiriwa wakasimanga.
Ee binti wa watu wangu, ujivike nguo ya magunia, na kugaagaa katika majivu; fanya maombolezo, kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, maombolezo ya uchungu mwingi; maana mwenye kuteka nyara atakuja juu yetu ghafla.
Kwa ajili ya hayo mwenye busara atanyamaza kimya wakati kama huo; kwa kuwa ni wakati mbaya.
Na mjomba wa mtu atakapomwinua, yaani, yeye amchomaye moto, ili atoe mifupa yake nyumbani, naye atakapomwambia yeye aliye katika pande za ndani za nyumba, Je! Yuko mtu yeyote pamoja nawe? Naye atakaposema, La, hapana; ndipo atasema, Nyamaza kimya; maana hatuna ruhusa kulitaja jina la BWANA.