Lakini mfalme akamwachilia Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo cha BWANA kilichokuwa kati yao, yaani, kati ya Daudi na Yonathani, mwana wa Sauli.
Mhubiri 8:2 - Swahili Revised Union Version Mimi nasema hivi, Uishike amri ya mfalme; na hiyo kwa sababu umeapa kwa Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tii amri ya mfalme, kwa sababu ya kiapo chako kitakatifu. Biblia Habari Njema - BHND Tii amri ya mfalme, kwa sababu ya kiapo chako kitakatifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tii amri ya mfalme, kwa sababu ya kiapo chako kitakatifu. Neno: Bibilia Takatifu Nawaambia, Tii amri ya mfalme, kwa sababu uliapa mbele za Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Nawaambia, Tii amri ya mfalme, kwa sababu uliapa mbele za Mungu. BIBLIA KISWAHILI Mimi nasema hivi, Uishike amri ya mfalme; na hiyo kwa sababu umeapa kwa Mungu. |
Lakini mfalme akamwachilia Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo cha BWANA kilichokuwa kati yao, yaani, kati ya Daudi na Yonathani, mwana wa Sauli.
Nao wakuu wote, na mashujaa, na wana wote wa mfalme Daudi nao, wakaahidi kuwa watiifu kwa mfalme Sulemani.
patakuwa na kiapo cha BWANA katikati ya watu hao wawili, kwamba alipeleka mkono wake kutwaa mali ya mwenziwe, na mwenyewe atakubali hayo, wala hatalipa.
Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa watawala na wenye mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema;
Na hapo watu walipoingia mwituni, tazama, hiyo asali ilikuwa ikidondoka; lakini hakuna mtu hata mmoja aliyetia mkono wake kinywani; kwa sababu hao watu walikuwa wakikiogopa kile kiapo.