Mhubiri 3:9 - Swahili Revised Union Version Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mfanyakazi hufaidi nini kutokana na juhudi zake hizo? Biblia Habari Njema - BHND Mfanyakazi hufaidi nini kutokana na juhudi zake hizo? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mfanyakazi hufaidi nini kutokana na juhudi zake hizo? Neno: Bibilia Takatifu Mfanyakazi anapata faida gani kutokana na taabu yake? Neno: Maandiko Matakatifu Mfanyakazi anapata faida gani kutokana na taabu yake? BIBLIA KISWAHILI Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo? |
Kisha nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; na tazama, yote ni ubatili na kufukuza upepo, wala faida hakuna chini ya jua.
Hiyo ndiyo balaa mbaya sana, ya kwamba kama vile alivyokuja, vivyo hivyo atakwenda zake; naye amefaidiwa nini mwenye kujitaabisha kwa ajili ya upepo?
Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kuipoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?