Yehu mwana wa Hanani mwonaji akatoka kwenda kumlaki, akamwambia mfalme Yehoshafati, Je! Imekupasa kuwasaidia waovu, na kuwapenda wamchukiao BWANA? Kwa ajili ya hayo ghadhabu itokayo kwa BWANA i juu yako.
Mhubiri 10:1 - Swahili Revised Union Version Nzi waliokufa hufanya manukato ya mwuza marashi kutoa uvundo; Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nzi waliokufa husababisha marashi kunuka; upumbavu kidogo hubatilisha hekima na heshima. Biblia Habari Njema - BHND Nzi waliokufa husababisha marashi kunuka; upumbavu kidogo hubatilisha hekima na heshima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nzi waliokufa husababisha marashi kunuka; upumbavu kidogo hubatilisha hekima na heshima. Neno: Bibilia Takatifu Kama vile inzi waliokufa huacha harufu mbaya kwenye manukato, ndivyo upumbavu kidogo huzidi nguvu hekima na heshima. Neno: Maandiko Matakatifu Kama vile nzi waliokufa huacha harufu mbaya kwenye manukato, ndivyo upumbavu kidogo huzidi nguvu hekima na heshima. BIBLIA KISWAHILI Nzi waliokufa hufanya manukato ya mwuza marashi kutoa uvundo; Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima. |
Yehu mwana wa Hanani mwonaji akatoka kwenda kumlaki, akamwambia mfalme Yehoshafati, Je! Imekupasa kuwasaidia waovu, na kuwapenda wamchukiao BWANA? Kwa ajili ya hayo ghadhabu itokayo kwa BWANA i juu yako.
Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; lakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.
Kwa sababu hii aliajiriwa, ili mimi niogope, nikafanye hivyo na kutenda dhambi, kisha wao wawe nazo habari mbaya, ili wanishutumie.
Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa bahari; Kwa hiyo maneno yangu yamekuwa ya haraka.
nawe utayafanya mafuta ya kutiwa matakatifu, marhamu iliyochanganywa kwa kazi ya ustadi ya mtengezaji manukato; yatakuwa ni mafuta matakatifu ya kutiwa.
Mtu akichukua nyama takatifu katika upindo wa nguo yake, naye kwa upindo wake akagusa mkate, au ugali, au divai, au mafuta, au chakula chochote, je, Kitu hicho kitakuwa kitakatifu? Makuhani wakajibu, wakasema, La.
Ndipo Hagai akasema, Kama mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti, akigusa kimojawapo cha vitu hivi, je, Kitakuwa najisi? Makuhani wakajibu, wakasema, Kitakuwa najisi.