Akazisimamisha nguzo ukumbini pa hekalu; akaisimamisha nguzo ya kulia, akaiita jina lake Yakini; akaisimamisha nguzo ya kushoto, akaiita jina lake Boazi.
Methali 9:1 - Swahili Revised Union Version Hekima ameijenga nyumba yake, Amezichonga nguzo zake saba; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hekima amejenga nyumba yake, nyumba yenye nguzo saba. Biblia Habari Njema - BHND Hekima amejenga nyumba yake, nyumba yenye nguzo saba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hekima amejenga nyumba yake, nyumba yenye nguzo saba. Neno: Bibilia Takatifu Hekima amejenga nyumba yake; amechonga nguzo zake saba. Neno: Maandiko Matakatifu Hekima amejenga nyumba yake; amechonga nguzo zake saba. BIBLIA KISWAHILI Hekima ameijenga nyumba yake, Amezichonga nguzo zake saba; |
Akazisimamisha nguzo ukumbini pa hekalu; akaisimamisha nguzo ya kulia, akaiita jina lake Yakini; akaisimamisha nguzo ya kushoto, akaiita jina lake Boazi.
Akaifanya baraza ya nguzo; mikono hamsini urefu wake, na mikono thelathini upana wake; na ukumbi mbele yake; na nguzo na mihimili minene mbele yake.
Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila gharama.
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
tena Yakobo, Kefa, na Yohana, waliosifika kuwa ni nguzo, walipoitambua ile neema niliyopewa, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kulia wa kuonesha ushirikiano; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;
Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.
Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.