Methali 8:4 - Swahili Revised Union Version Enyi watu, nawaita ninyi; Na sauti yangu ni kwa wanadamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Enyi watu wote, nawaita nyinyi! Wito wangu ni kwa ajili ya binadamu. Biblia Habari Njema - BHND “Enyi watu wote, nawaita nyinyi! Wito wangu ni kwa ajili ya binadamu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Enyi watu wote, nawaita nyinyi! Wito wangu ni kwa ajili ya binadamu. Neno: Bibilia Takatifu “Ni ninyi watu, ninaowaita; ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote. Neno: Maandiko Matakatifu “Ni ninyi wanaume, ninaowaita; ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote. BIBLIA KISWAHILI Enyi watu, nawaita ninyi; Na sauti yangu ni kwa wanadamu. |
Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini, Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele.
Sikilizeni, enyi watu wa kabila zote; sikiliza, Ee dunia, na vyote vilivyomo; Bwana MUNGU na ashuhudie juu yenu, yeye Bwana kutoka hekalu lake takatifu.
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa kwa viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nilikuwa mhudumu wake.
ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo.
Roho na Bibi arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.