Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila kiumbe kitambaacho nchini.
Methali 8:23 - Swahili Revised Union Version Nilitukuka tokea milele, tangu awali, Kabla haijakuwako dunia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilifanywa mwanzoni mwa nyakati, nilikuwako kabla ya dunia kuanza. Biblia Habari Njema - BHND Nilifanywa mwanzoni mwa nyakati, nilikuwako kabla ya dunia kuanza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilifanywa mwanzoni mwa nyakati, nilikuwako kabla ya dunia kuanza. Neno: Bibilia Takatifu niliteuliwa tangu milele, tangu mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa. Neno: Maandiko Matakatifu niliteuliwa tangu milele, tangu mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa. BIBLIA KISWAHILI Nilitukuka tokea milele, tangu awali, Kabla haijakuwako dunia. |
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila kiumbe kitambaacho nchini.
Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.
Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye asili yake imekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.
Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.