Mika 5:2 - Swahili Revised Union Version2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye asili yake imekuwa tangu zamani za kale, tangu milele. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema2 Mwenyezi-Mungu asema, “Lakini wewe Bethlehemu katika Efratha, wewe ni mdogo tu kati ya jamii za Yuda, lakini kwako kutatoka mtawala atakayetawala juu ya Israeli kwa niaba yangu. Asili yake ni ya zama za kale.” Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND2 Mwenyezi-Mungu asema, “Lakini wewe Bethlehemu katika Efratha, wewe ni mdogo tu kati ya jamii za Yuda, lakini kwako kutatoka mtawala atakayetawala juu ya Israeli kwa niaba yangu. Asili yake ni ya zama za kale.” Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza2 Hivyo Mungu atawaacha watu wake kwa maadui, mpaka yule mama mjamzito atakapojifungua. Kisha ndugu zake waliobakia, watarudi na kuungana na Waisraeli wenzao. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu2 “Lakini wewe, Bethlehemu Efrata, ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda, kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli, ambaye asili yake ni kutoka zamani, kutoka milele.” Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu2 “Lakini wewe, Bethlehemu Efrathi, ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda, kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli, ambaye asili yake ni kutoka zamani, kutoka milele.” Tazama suraBIBLIA KISWAHILI2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye asili yake imekuwa tangu zamani za kale, tangu milele. Tazama sura |