Methali 8:1 - Swahili Revised Union Version Je! Hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sikilizeni! Hekima anaita! Busara anapaza sauti yake! Biblia Habari Njema - BHND Sikilizeni! Hekima anaita! Busara anapaza sauti yake! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sikilizeni! Hekima anaita! Busara anapaza sauti yake! Neno: Bibilia Takatifu Je, hekima haitani? Je, ufahamu hapazi sauti? Neno: Maandiko Matakatifu Je, hekima haitani? Je, ufahamu hapazi sauti? BIBLIA KISWAHILI Je! Hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake? |
Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.
Katika siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na kote katika Yudea, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wagiriki, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.