Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lolote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu.
Methali 30:7 - Swahili Revised Union Version Mambo haya mawili nimekuomba; Usininyime [matatu] kabla sijafa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mambo haya mawili nakuomba ee Mungu, wala usinikatalie kabla sijafa: Biblia Habari Njema - BHND Mambo haya mawili nakuomba ee Mungu, wala usinikatalie kabla sijafa: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mambo haya mawili nakuomba ee Mungu, wala usinikatalie kabla sijafa: Neno: Bibilia Takatifu “Ninakuomba vitu viwili, Ee Mwenyezi Mungu; usininyime kabla sijafa: Neno: Maandiko Matakatifu “Ninakuomba vitu viwili, Ee bwana; usininyime kabla sijafa: BIBLIA KISWAHILI Mambo haya mawili nimekuomba; Usininyime [matatu] kabla sijafa. |
Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lolote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu.
Neno moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni mwake.
Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.
lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hatanyang'anywa.