Methali 3:17 - Swahili Revised Union Version Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Njia zake ni za kupendeza, zote zaelekea kwenye amani. Biblia Habari Njema - BHND Njia zake ni za kupendeza, zote zaelekea kwenye amani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Njia zake ni za kupendeza, zote zaelekea kwenye amani. Neno: Bibilia Takatifu Njia zake zinapendeza, mapito yake yote ni amani. Neno: Maandiko Matakatifu Njia zake zinapendeza, mapito yake yote ni amani. BIBLIA KISWAHILI Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani. |
Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.
Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.
Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.
Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na muwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,