Methali 29:16 - Swahili Revised Union Version Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka; Bali wenye haki watayatazama maanguko yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waovu wakitawala maovu huongezeka, lakini waadilifu watashuhudia kuanguka kwao. Biblia Habari Njema - BHND Waovu wakitawala maovu huongezeka, lakini waadilifu watashuhudia kuanguka kwao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waovu wakitawala maovu huongezeka, lakini waadilifu watashuhudia kuanguka kwao. Neno: Bibilia Takatifu Waovu wanapostawi, dhambi huongezeka pia; lakini wenye haki wataliona anguko lao. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati waovu wanapostawi, pia dhambi vivyo hivyo, lakini wenye haki wataliona anguko lao. BIBLIA KISWAHILI Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka; Bali wenye haki watayatazama maanguko yao. |
Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Utawaona Wasio haki wakiangamizwa.
Na jicho langu limeona kuanguka kwa adui zangu, Sikio langu limesikia maangamizi ya waovu walionishambulia.
Maana hao adui zako, Ee BWANA, Hao adui zako watapotea, Na watendao maovu watatawanyika wote pia.
Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.
Furahini juu yake, enyi mbingu, na enyi watakatifu, mitume na manabii; kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.