Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Methali 28:2 - Swahili Revised Union Version

Kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi; Bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Taifa la fujo huzusha viongozi wengi, lakini kwa kiongozi mmoja mwenye akili na maarifa huwa na utengemano

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Taifa la fujo huzusha viongozi wengi, lakini kwa kiongozi mmoja mwenye akili na maarifa huwa na utengemano

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Taifa la fujo huzusha viongozi wengi, lakini kwa kiongozi mmoja mwenye akili na maarifa huwa na utengemano

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Nchi inapokuwa na uasi, inakuwa na viongozi wengi, bali kiongozi mwenye ufahamu na maarifa hudumisha utaratibu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Wakati nchi inapokuwa na uasi, inakuwa na viongozi wengi, bali mwenye ufahamu na maarifa hudumisha utaratibu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi; Bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa

Tazama sura
Tafsiri zingine

Methali 28:2
14 Marejeleo ya Msalaba  

Nadabu mwana wa Yeroboamu alianza kutawala juu ya Israeli, mwaka wa pili wa Asa mfalme wa Yuda, akatawala juu ya Israeli miaka miwili.

Mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda Baasha akamwua, akatawala mahali pake.

Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki; Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu.

Basi, kulikuwemo na mtu maskini mwenye hekima, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule lakini hata hivyo hapakuwa na mtu yeyote aliyemkumbuka yule mtu maskini.

Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejesha njia za kukaa.

Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; uache dhambi zako kwa kutenda haki, uache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za fanaka.

Nimekupa mfalme katika hasira yangu, nikamwondoa katika ghadhabu yangu.