Kwa maana vita vilienea huko juu ya uso wote wa nchi; na siku ile huo msitu ukala watu wengi kuliko wale walioliwa na upanga.
Methali 24:21 - Swahili Revised Union Version Mwanangu, mche BWANA, na mfalme; Wala usishirikiane na wenye kigeugeu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwanangu, umche Mwenyezi-Mungu na kumheshimu mfalme, wala usishirikiane na wale wasio na msimamo, Biblia Habari Njema - BHND Mwanangu, umche Mwenyezi-Mungu na kumheshimu mfalme, wala usishirikiane na wale wasio na msimamo, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwanangu, umche Mwenyezi-Mungu na kumheshimu mfalme, wala usishirikiane na wale wasio na msimamo, Neno: Bibilia Takatifu Mwanangu, mche Mwenyezi Mungu na mfalme, wala usijiunge na waasi, Neno: Maandiko Matakatifu Mwanangu, mche bwana na mfalme, wala usijiunge na waasi, BIBLIA KISWAHILI Mwanangu, mche BWANA, na mfalme; Wala usishirikiane na wenye kigeugeu; |
Kwa maana vita vilienea huko juu ya uso wote wa nchi; na siku ile huo msitu ukala watu wengi kuliko wale walioliwa na upanga.
Ndipo wageni wote waliokuwa pamoja na Adonia wakaogopa, wakaondoka, wakaenda zao kila mtu njia yake.
Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hakuwasikia, hao watu walimjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya! Nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi. Hivyo Israeli wakaenda zao hemani kwao.
Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya BWANA juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha BWANA, wakamwamini BWANA, na Musa mtumishi wake.
Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.
Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa watawala na wenye mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema;
Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili, kuunyosha mkono wangu juu yake, kwa maana yeye ni masihi wa BWANA.