Methali 24:11 - Swahili Revised Union Version Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwokoe mtu anayechukuliwa kuuawa bure; usisite kumwokoa anayeuawa bila hatia. Biblia Habari Njema - BHND Mwokoe mtu anayechukuliwa kuuawa bure; usisite kumwokoa anayeuawa bila hatia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwokoe mtu anayechukuliwa kuuawa bure; usisite kumwokoa anayeuawa bila hatia. Neno: Bibilia Takatifu Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo; wazuie wote wanaojikokota kuelekea machinjoni. Neno: Maandiko Matakatifu Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo; wazuie wote wanaojikokota kuelekea machinjoni. BIBLIA KISWAHILI Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe. |
Nimeteswa tangu ujana wangu na niko karibu kufa, Nimeumia kwa mapigo yako; nami nimekata tamaa.
Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tuko hapa.
Nao wote wakamshika Sosthene, mkuu wa sinagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu. Wala Galio hakuyaona mambo hayo kuwa ni kitu.
Ugomvi mkubwa ulipotokea, yule jemadari akahofia Paulo asije akararuliwa nao, akaamuru askari washuke na kumwondoa kwa nguvu mikononi mwao, na kumleta ndani ya ngome.