Methali 24:10 - Swahili Revised Union Version Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ukifa moyo wakati wa shida, basi wewe ni dhaifu kweli. Biblia Habari Njema - BHND Ukifa moyo wakati wa shida, basi wewe ni dhaifu kweli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ukifa moyo wakati wa shida, basi wewe ni dhaifu kweli. Neno: Bibilia Takatifu Ukikata tamaa wakati wa taabu, jinsi gani nguvu zako ni kidogo! Neno: Maandiko Matakatifu Ukikata tamaa wakati wa taabu, jinsi gani nguvu zako ni kidogo! BIBLIA KISWAHILI Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache. |
Wala isizimie mioyo yenu, wala msiiogope habari itakayosikiwa katika nchi; maana habari itakuja mwaka mmoja, na baadaye mwaka wa pili habari itakuja, na udhalimu katika nchi, mwenye kutawala akishindana na mwenye kutawala.
Basi naomba msikate tamaa kwa sababu ya dhiki zangu kwa ajili yenu, zilizo utukufu wenu.
Tena maofisa na waseme zaidi na watu, wawaambie, Ni mtu gani aliye hapa tena mwenye hofu na moyo mnyonge? Aende akarudi nyumbani kwake, isije mioyo ya nduguze ikayeyuka mfano wa moyo wake.
Ninapajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe unalishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.
Ndipo Daudi aliposema moyoni mwake, Siku moja, basi, mimi nitaangamia kwa mkono wa Sauli; hakuna jema zaidi kwangu kuliko kukimbia mpaka nchi ya Wafilisti; naye Sauli atakata tamaa kunihusu, asinitafute tena kote mipakani mwa Israeli; hivyo nitaokoka katika mikono yake.