Methali 23:35 - Swahili Revised Union Version Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utasema, “Walinichapa, lakini sikuumia; walinipiga, lakini sina habari. Nitaamka lini? Ngoja nitafute kinywaji kingine!” Biblia Habari Njema - BHND Utasema, “Walinichapa, lakini sikuumia; walinipiga, lakini sina habari. Nitaamka lini? Ngoja nitafute kinywaji kingine!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utasema, “Walinichapa, lakini sikuumia; walinipiga, lakini sina habari. Nitaamka lini? Ngoja nitafute kinywaji kingine!” Neno: Bibilia Takatifu Utasema, “Wamenipiga lakini sikuumia! Wamenichapa, lakini sisikii! Nitaamka lini ili nikanywe tena?” Neno: Maandiko Matakatifu Utasema, “Wamenipiga lakini sikuumia! Wamenichapa, lakini sisikii! Nitaamka lini ili nikanywe tena?” BIBLIA KISWAHILI Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena. |
na kumbe! Furaha, na kuchekelea, na kuchinja ng'ombe, na kuchinja kondoo, na kula nyama, na kunywa mvinyo; tule, tunywe, kwa maana kesho tutakufa.
Husema, Njooni, nitaleta divai, Na tunywe sana kileo; Na kesho itakuwa kama leo, Sikukuu kupita kiasi.
Hakika nimemsikia Efraimu, akijililia hivi, Umeniadhibu, nami nikaadhibika, kama ndama asiyeizoea nira; unigeuze, nami nitageuka; kwa maana wewe u BWANA, Mungu wangu.
Ee BWANA, macho yako je! Hayaangalii uaminifu? Umewapiga, lakini hawakuhuzunika; umewakomesha, lakini wamekataa kurudiwa wamefanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba wamekataa kurudi.
ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani.
ikawa asikiapo maneno ya laana hii, ajibarikie mtu huyo moyoni mwake, na kusema, Nitakuwa katika amani, nijapotembea katika upotoe wa moyo wangu kwa kuangamiza mbichi na kavu;
Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaagaa matopeni.