Methali 22:8 - Swahili Revised Union Version Yeye apandaye uovu atavuna msiba, Na fimbo ya ghadhabu yake itakoma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Apandaye dhuluma atavuna janga; uwezo wake wa kutenda mabaya utavunjwa. Biblia Habari Njema - BHND Apandaye dhuluma atavuna janga; uwezo wake wa kutenda mabaya utavunjwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Apandaye dhuluma atavuna janga; uwezo wake wa kutenda mabaya utavunjwa. Neno: Bibilia Takatifu Yeye aupandaye uovu huvuna taabu, nayo fimbo ya ghadhabu yake itaangamizwa. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye aupandaye uovu huvuna taabu, nayo fimbo ya ghadhabu yake itaangamizwa. BIBLIA KISWAHILI Yeye apandaye uovu atavuna msiba, Na fimbo ya ghadhabu yake itakoma. |
Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya nchi ya wenye haki; Ili wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu.
Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi.
Ole wake Ashuru! Fimbo ya hasira yangu, ambaye gongo lililo mkononi mwake ni ghadhabu yangu!
Msifurahi, Enyi Wafilisti wote, Kwa sababu fimbo ile iliyokupiga imevunjika; Maana katika shina la nyoka atatoka fira, Na uzao wake ni joka la moto arukaye Sef 2:4-7; Zek 9:5-7
Kwa maana umeivunja nira ya mzigo wake, na gongo la bega lake, na fimbo yake yeye aliyemwonea, kama katika siku ya Midiani.
Mmelima dhuluma, mmevuna uovu; mmekula matunda ya uongo; kwa maana uliitumainia njia yako, na wingi wa mashujaa wako.
Kwa maana wao hupanda upepo, nao watavuna tufani; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza.