Kwa maana nimemchagua ili awaamuru wanawe na vizazi vyake baada yake wadumishe njia ya BWANA, kwa kuwa wenye haki na kweli, ili BWANA naye akamtimizie Abrahamu ahadi zake.
Methali 22:6 - Swahili Revised Union Version Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mfunze mtoto namna ya kuishi vizuri, naye hatasahau njia hiyo hata uzeeni. Biblia Habari Njema - BHND Mfunze mtoto namna ya kuishi vizuri, naye hatasahau njia hiyo hata uzeeni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mfunze mtoto namna ya kuishi vizuri, naye hatasahau njia hiyo hata uzeeni. Neno: Bibilia Takatifu Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea, naye hataiacha hata akiwa mzee. Neno: Maandiko Matakatifu Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea, naye hataiacha hata akiwa mzee. BIBLIA KISWAHILI Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. |
Kwa maana nimemchagua ili awaamuru wanawe na vizazi vyake baada yake wadumishe njia ya BWANA, kwa kuwa wenye haki na kweli, ili BWANA naye akamtimizie Abrahamu ahadi zake.
Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.
Nayo wafunzeni watoto wenu kwa kuyazungumza uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;
nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyasema uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
na ya kuwa tangu utotoni umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
Manoa akasema, Basi sasa hayo maneno yako yatakapotimia, je! Huyo mtoto atakuwa wa namna gani, na kazi yake itakuwa ni nini?
kwa sababu hiyo mimi nami nimempa BWANA mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa BWANA. Naye akamwabudu BWANA huko.