Methali 20:24 - Swahili Revised Union Version Mwenendo wa mtu watoka kwa BWANA; Basi, awezaje mtu kuelewa na njia yake? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hatua za mtu huongozwa na Mwenyezi-Mungu; awezaje binadamu kujua njia ya kwenda? Biblia Habari Njema - BHND Hatua za mtu huongozwa na Mwenyezi-Mungu; awezaje binadamu kujua njia ya kwenda? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hatua za mtu huongozwa na Mwenyezi-Mungu; awezaje binadamu kujua njia ya kwenda? Neno: Bibilia Takatifu Hatua za mtu huongozwa na Mwenyezi Mungu. Anawezaje basi mtu yeyote kuelewa njia yake mwenyewe? Neno: Maandiko Matakatifu Hatua za mtu huongozwa na bwana. Anawezaje basi mtu yeyote kuelewa njia yake mwenyewe? BIBLIA KISWAHILI Mwenendo wa mtu watoka kwa BWANA; Basi, awezaje mtu kuelewa na njia yake? |
Ee BWANA, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu.
Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lolote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza.
Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazawa wake.