Ulimwengu wote ukamtafuta Sulemani uso wake, ili waisikie hekima yake, Mungu aliyomtia moyoni.
Methali 2:6 - Swahili Revised Union Version Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana Mwenyezi-Mungu huwapa watu hekima; kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. Biblia Habari Njema - BHND Maana Mwenyezi-Mungu huwapa watu hekima; kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana Mwenyezi-Mungu huwapa watu hekima; kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana Mwenyezi Mungu hutoa hekima, na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana bwana hutoa hekima, na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; |
Ulimwengu wote ukamtafuta Sulemani uso wake, ili waisikie hekima yake, Mungu aliyomtia moyoni.
basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.
Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu watu hawa wako walio wengi?
Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani.
BWANA na akupe busara na akili, akakuagizie juu ya Israeli; ili uishike Torati ya BWANA, Mungu wako.
Na wewe, Ezra, kwa kadiri ya hekima ya Mungu wako iliyo mkononi mwako, waweke mahakimu na majaji, watakaowaamua watu wote walio ng'ambo ya Mto, yaani, wote wenye kuzijua amri za Mungu wako; na ukamfundishe yeye asiyezijua.
Mungu wangu akanitia moyoni mwangu, kwamba niwakusanye wakuu na maofisa, na watu, ili wahesabiwe kwa nasaba. Nikakiona kitabu cha vizazi vya hao waliokwea hapo kwanza, nikaona ya kwamba imeandikwa humo;
Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako.
Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia hekima mtu asiye nayo.
Maagizo ya BWANA ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya BWANA ni safi, Huyatia macho nuru.
nami nimemjaza Roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,
Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.
Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.
Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi kulingana na neno hili, bila shaka kwa hao hakuna asubuhi.
Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.
Yeye hubadili majira na nyakati; hutengua na kuteua wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa;
Nakushukuru, nakuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu, uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliyotaka kwako; maana umetujulisha neno lile la mfalme.
kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.
Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu.
Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.