Nami leo nimedhoofika, hata nijapotiwa mafuta niwe mfalme; na watu hao, wana wa Seruya, ni wagumu kwangu mimi; BWANA amlipie mwovu kulingana na uovu wake.
Methali 19:10 - Swahili Revised Union Version Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu; Sembuse mtumwa awatawale wakuu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Haifai kwa mpumbavu kuishi kwa anasa, tena ni vibaya zaidi mtumwa kuwatawala wakuu. Biblia Habari Njema - BHND Haifai kwa mpumbavu kuishi kwa anasa, tena ni vibaya zaidi mtumwa kuwatawala wakuu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Haifai kwa mpumbavu kuishi kwa anasa, tena ni vibaya zaidi mtumwa kuwatawala wakuu. Neno: Bibilia Takatifu Haistahili mpumbavu kuishi katika anasa, itakuwa vibaya kiasi gani kwa mtumwa kuwatawala wakuu. Neno: Maandiko Matakatifu Haistahili mpumbavu kuishi katika anasa, itakuwa vibaya kiasi gani kwa mtumwa kuwatawala wakuu. BIBLIA KISWAHILI Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu; Sembuse mtumwa awatawale wakuu. |
Nami leo nimedhoofika, hata nijapotiwa mafuta niwe mfalme; na watu hao, wana wa Seruya, ni wagumu kwangu mimi; BWANA amlipie mwovu kulingana na uovu wake.
Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai; bali mji wa Shushani ukafadhaika.
Maneno mazuri hayapendezi kinywani mwa mpumbavu; Sembuse midomo ya uongo kinywani mwa mkuu.
Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno; Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu.
Nao watu wataonewa, kila mtu na mwenziwe, na kila mtu na jirani yake; mtoto atajivuna mbele ya mzee, na mtu mnyonge mbele ya mtu mwenye heshima.
Usifurahi, Israeli, kwa sababu ya furaha, kama hao mataifa; kwa kuwa umezini juu ya Mungu wako, umependa ujira katika kila sakafu ya nafaka.
Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Abrahamu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni kubwa.
Kisha Abigaili alimjia Nabali; na tazama, alikuwa amefanya karamu nyumbani mwake, kama karamu ya kifalme; na moyo wake huyo Nabali ukafurahiwa ndani yake, kwa maana amelewa kabisa. Kwa sababu hiyo hakumwambia neno, dogo wala kubwa, hadi kulipopambazuka.