Methali 16:3 - Swahili Revised Union Version Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatakuwa kweli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako, nayo mipango yako itafanikiwa. Biblia Habari Njema - BHND Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako, nayo mipango yako itafanikiwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako, nayo mipango yako itafanikiwa. Neno: Bibilia Takatifu Mkabidhi Mwenyezi Mungu lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa. Neno: Maandiko Matakatifu Mkabidhi bwana lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa. BIBLIA KISWAHILI Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatakuwa kweli. |
Akawaambia wanafunzi wake, Kwa sababu hiyo nawaambia, Msisumbukie maisha yenu, mtakula nini; wala miili yenu, mtavaa nini.
Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.