Methali 12:6 - Swahili Revised Union Version Maneno ya waovu huotea damu; Bali kinywa cha wanyofu kitawaokoa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maneno ya waovu lengo lake ni kuua, lakini maneno ya waadilifu huwaokoa wanaotishwa. Biblia Habari Njema - BHND Maneno ya waovu lengo lake ni kuua, lakini maneno ya waadilifu huwaokoa wanaotishwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maneno ya waovu lengo lake ni kuua, lakini maneno ya waadilifu huwaokoa wanaotishwa. Neno: Bibilia Takatifu Maneno ya waovu huotea kumwaga damu, bali maneno ya waadilifu huwaokoa. Neno: Maandiko Matakatifu Maneno ya waovu huotea kumwaga damu, bali maneno ya waadilifu huwaokoa. BIBLIA KISWAHILI Maneno ya waovu huotea damu; Bali kinywa cha wanyofu kitawaokoa. |
Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi.
Miguu yao hukimbilia mabaya, nao hufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia zao kuu.
Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huvizia kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu.
Kulipopambazuka, Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hadi wamwue Paulo.
Basi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua habari zake vizuri zaidi; na sisi tuko tayari kumwua kabla hajakaribia.
na kumwomba fadhili juu yake, kwamba atoe amri aletwe Yerusalemu, wapate kumwotea na kumwua njiani.