bali mfalme alipoarifiwa, aliamuru kwa barua ya kwamba huo mpango mwovu alioufanya juu ya Wayahudi umrudie kichwani pake mwenyewe; na ya kwamba yeye na wanawe watundikwe juu ya mti.
Methali 11:16 - Swahili Revised Union Version Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; Na watu wakali hushika mali siku zote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwanamke mwema huheshimiwa, mwanamume mwenye bidii hutajirika. Biblia Habari Njema - BHND Mwanamke mwema huheshimiwa, mwanamume mwenye bidii hutajirika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwanamke mwema huheshimiwa, mwanamume mwenye bidii hutajirika. Neno: Bibilia Takatifu Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata heshima, bali wanaume wakorofi hupata mali tu. Neno: Maandiko Matakatifu Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata heshima, bali wanaume wakorofi hupata mali tu. BIBLIA KISWAHILI Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; Na watu wakali hushika mali siku zote. |
bali mfalme alipoarifiwa, aliamuru kwa barua ya kwamba huo mpango mwovu alioufanya juu ya Wayahudi umrudie kichwani pake mwenyewe; na ya kwamba yeye na wanawe watundikwe juu ya mti.
Kwa maana hawajui kutenda haki, asema BWANA, hao wawekao akiba ya jeuri na unyang'anyi katika majumba yao.
Tangazeni habari katika majumba ya Ashdodi, na katika majumba ya nchi ya Misri, mkaseme, Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria, katazameni, ni mishindo mikubwa kama nini iliyomo humo, na udhalimu mwingi kama nini uliomo ndani yake.
Amin, nawaambieni, Kila patakapohubiriwa Injili hii katika ulimwengu wote, tendo hilo alilolitenda huyu litatajwa pia kwa kumbukumbu yake.
lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hatanyang'anywa.
na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.
Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu ghorofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao.
Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuayo ile kweli;
Na hao watumishi wa Daudi walipomjia huyo Abigaili huko Karmeli, walimwambia, wakasema, Daudi ametutuma kwako ili tukutwae uwe mkewe.