Methali 1:4 - Swahili Revised Union Version Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na tahadhari; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huwapatia wajinga werevu na vijana maarifa na hadhari. Biblia Habari Njema - BHND Huwapatia wajinga werevu na vijana maarifa na hadhari. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huwapatia wajinga werevu na vijana maarifa na hadhari. Neno: Bibilia Takatifu huwapa busara wajinga, maarifa na akili kwa vijana; Neno: Maandiko Matakatifu huwapa busara wajinga, maarifa na akili kwa vijana; BIBLIA KISWAHILI Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na tahadhari; |
Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia hekima mtu asiye nayo.
Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na kinachotamaniwa na macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.
Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.
Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili.
Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.