Methali 1:27 - Swahili Revised Union Version Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema hofu itakapowakumba kama tufani, maafa yenu yatakapowavamia kama kimbunga, wakati udhia na dhiki vitakapowapata. Biblia Habari Njema - BHND hofu itakapowakumba kama tufani, maafa yenu yatakapowavamia kama kimbunga, wakati udhia na dhiki vitakapowapata. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza hofu itakapowakumba kama tufani, maafa yenu yatakapowavamia kama kimbunga, wakati udhia na dhiki vitakapowapata. Neno: Bibilia Takatifu janga litakapowapata kama tufani, maafa yatakapowazoa kama upepo wa kisulisuli, dhiki na taabu zitakapowalemea. Neno: Maandiko Matakatifu wakati janga litawapata kama tufani, wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli, wakati dhiki na taabu zitawalemea. BIBLIA KISWAHILI Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia. |
Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba, Ataipeperusha kama chamchela, Iliyo mibichi na iliyo moto.
Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana, Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo, Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani.
Tazama, tufani ya BWANA, yaani, ghadhabu yake, imetokea; ni kimbunga cha tufani; itapasuka, na kuwaangukia waovu vichwani.
BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.
dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Mgiriki pia;
Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.