Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Nahumu 1:3 - Swahili Revised Union Version

3 BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Mwenyezi-Mungu hakasiriki upesi, lakini amejaa nguvu, Mwenyezi-Mungu kamwe hatawaachilia wenye hatia. Apitapo Mwenyezi-Mungu, huzuka kimbunga na dhoruba; mawingu ni vumbi litimuliwalo na nyayo zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Mwenyezi-Mungu hakasiriki upesi, lakini amejaa nguvu, Mwenyezi-Mungu kamwe hatawaachilia wenye hatia. Apitapo Mwenyezi-Mungu, huzuka kimbunga na dhoruba; mawingu ni vumbi litimuliwalo na nyayo zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Mwenyezi-Mungu hakasiriki upesi, lakini amejaa nguvu, Mwenyezi-Mungu kamwe hatawaachilia wenye hatia. Apitapo Mwenyezi-Mungu, huzuka kimbunga na dhoruba; mawingu ni vumbi litimuliwalo na nyayo zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Mwenyezi Mungu si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu, Mwenyezi Mungu hataacha kuadhibu wenye hatia. Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni vumbi la miguu yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 bwana si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu, bwana hataacha kuadhibu wenye hatia. Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni vumbi la miguu yake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.

Tazama sura Nakili




Nahumu 1:3
33 Marejeleo ya Msalaba  

Aliziinamisha mbingu akashuka; Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.


ila wakakataa kutii, wala hawakuyakumbuka maajabu yako, uliyoyafanya kati yao; lakini wakafanya shingo zao kuwa ngumu, na katika kuasi kwao wakaweka jemadari, ili wairudie hali ya utumwa; lakini wewe u Mungu, uliye tayari kusamehe, mwenye neema, mwenye huruma nyingi, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, basi hukuwaacha.


Nikifanya dhambi, ndipo waniangalia, Wala hutaniachilia na uovu wangu.


Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,


Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu; Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa?


BWANA amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.


Na kuziweka nguzo za ghorofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, Na kwenda juu ya mabawa ya upepo,


BWANA ni mwenye fadhili na huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,


Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, Akili zake hazina mpaka.


Mungu wetu atakuja wala sio kimya kimya, Moto utakula mbele zake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote.


Mara moja amenena Mungu; Mara mbili nimeyasikia haya, Ya kuwa nguvu zina Mungu,


Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini! Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.


Ufunuo juu ya Misri. Tazama, BWANA amepanda juu ya wingu jepesi, anafika Misri; na sanamu za Misri zinatikisika mbele zake, na moyo wa Misri unayeyuka ndani yake.


Naye atajiliwa na BWANA wa majeshi kwa ngurumo, na tetemeko la nchi, na sauti kuu, na chamchela, na tufani, na mwali wa moto uteketezao.


Maana BWANA atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto.


Tazama atapanda juu kama mawingu, na magari yake ya vita yatakuwa kama kisulisuli; farasi wake ni wepesi kuliko tai. Ole wetu, kwa sababu tumeharibika.


Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.


Kwa maana wao hupanda upepo, nao watavuna tufani; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza.


rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi kuadhibu.


Akamwomba BWANA, akasema, Nakuomba, Ee BWANA; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? Hii ndiyo sababu nilifanya haraka kukimbilia Tarshishi; kwa maana nilijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, nawe waghairi mabaya.


Naye BWANA ataonekana juu yao, Na mshale wake utatoka kama umeme; Na Bwana MUNGU ataipiga tarumbeta, Naye atakwenda kwa pepo za kisulisuli za kusini.


BWANA ni mpole wa hasira, mwingi wa rehema, mwenye kusamehe uovu na makosa, naye hatamfanya mwenye hatia kuwa hana makosa kwa njia yoyote; mwenye kuwapatiliza wana kwa uovu wa baba zao, katika kizazi cha tatu na cha nne.


Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi katika mkono wa kulia wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.


Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;


Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na makabila yote ya dunia yataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo