Methali 1:13 - Swahili Revised Union Version Tutapata mali yote ya thamani, Tutazijaza nyumba zetu mateka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tutajitwalia mali zote za thamani, nyumba zetu tutazijaza nyara. Biblia Habari Njema - BHND Tutajitwalia mali zote za thamani, nyumba zetu tutazijaza nyara. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tutajitwalia mali zote za thamani, nyumba zetu tutazijaza nyara. Neno: Bibilia Takatifu Tutapata aina zote za vitu vya thamani na kujaza nyumba zetu kwa nyara. Neno: Maandiko Matakatifu Tutapata aina zote za vitu vya thamani na kujaza nyumba zetu kwa nyara. BIBLIA KISWAHILI Tutapata mali yote ya thamani, Tutazijaza nyumba zetu mateka. |
Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi.
Kwa maana hawajui kutenda haki, asema BWANA, hao wawekao akiba ya jeuri na unyang'anyi katika majumba yao.
Tangazeni habari katika majumba ya Ashdodi, na katika majumba ya nchi ya Misri, mkaseme, Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria, katazameni, ni mishindo mikubwa kama nini iliyomo humo, na udhalimu mwingi kama nini uliomo ndani yake.
Simba alirarua vipande vipande chakula cha kuwatosha watoto wake, aliwakamatia majike wake mawindo, aliyajaza mapango yake mateka, na makao yake aliyajaza nyama iliyoraruliwa.
Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema BWANA wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema BWANA wa majeshi.
Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.