Mathayo 5:42 - Swahili Revised Union Version Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akuombaye mpe, wala usimpe kisogo anayetaka kukukopa kitu. Biblia Habari Njema - BHND Akuombaye mpe, wala usimpe kisogo anayetaka kukukopa kitu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akuombaye mpe, wala usimpe kisogo anayetaka kukukopa kitu. Neno: Bibilia Takatifu Mpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie kisogo yeye atakaye kukukopa. Neno: Maandiko Matakatifu Mpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie kisogo yeye atakaye kukukopa. BIBLIA KISWAHILI Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo. |
Asubuhi panda mbegu zako, Wala jioni usiulegeze mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa, kama ni hii au hii, au kama zote zitafaa sawasawa.
Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; uache dhambi zako kwa kutenda haki, uache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za fanaka.
Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.
Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia.
Dini iliyo safi, isiyo na dosari mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.