Walipokuwa wakitoka, wakamwona mtu Mkirene, jina lake Simoni; huyu wakamshurutisha auchukue msalaba wake.
Mathayo 5:41 - Swahili Revised Union Version Mtu yeyote akikulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye maili mbili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili. Biblia Habari Njema - BHND Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili. Neno: Bibilia Takatifu Mtu akikulazimisha kwenda maili moja, nenda naye maili mbili. Neno: Maandiko Matakatifu Kama mtu akikulazimisha kwenda maili moja, nenda naye maili mbili. BIBLIA KISWAHILI Mtu yeyote akikulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye maili mbili. |
Walipokuwa wakitoka, wakamwona mtu Mkirene, jina lake Simoni; huyu wakamshurutisha auchukue msalaba wake.
Wakamshurutisha mtu aliyekuwa akipita, akitoka mashambani, Simoni Mkirene, baba yao Iskanda na Rufo, ili auchukue msalaba wake.
Na walipokuwa wakimwondoa walimkamata mtu mmoja, Simoni Mkirene, aliyekuwa ametoka shambani, wakamtwika msalaba, auchukue nyuma yake Yesu.
Maana, upendo wa Kristo watuongoza; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote;