Je! Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu;
Mathayo 5:26 - Swahili Revised Union Version Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hadi utakapolipa senti ya mwisho. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kweli nakuambia, hutatoka humo mpaka umelipa senti ya mwisho. Biblia Habari Njema - BHND Kweli nakuambia, hutatoka humo mpaka umelipa senti ya mwisho. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kweli nakuambia, hutatoka humo mpaka umelipa senti ya mwisho. Neno: Bibilia Takatifu Amin, nakuambia, hutatoka humo hadi uwe umelipa senti ya mwisho. Neno: Maandiko Matakatifu Amin, nakuambia, hautatoka humo hadi uwe umelipa senti ya mwisho. BIBLIA KISWAHILI Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hadi utakapolipa senti ya mwisho. |
Je! Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu;
Kisha atawaambia na wale walioko katika mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
Maana, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidii kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya hakimu; yule hakimu akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani.
Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;