Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Mathayo 4:22 - Swahili Revised Union Version Mara wakaiacha mashua na baba yao, wakamfuata. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata. Biblia Habari Njema - BHND nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata. Neno: Bibilia Takatifu Nao mara moja wakaiacha mashua yao, pamoja na baba yao, wakamfuata. Neno: Maandiko Matakatifu Nao mara wakaiacha mashua yao, pamoja na baba yao, wakamfuata. BIBLIA KISWAHILI Mara wakaiacha mashua na baba yao, wakamfuata. |
Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Alipoendelea, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwa katika mashua pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita.
Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila namna waliyokuwa nayo watu.
Mara akawaita, wakamwacha baba yao Zebedayo ndani ya mashua pamoja na wafanya kazi wakaenda, wakamfuata.
Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake wa kiume na wa kike; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.