Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arubaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.
Mathayo 4:2 - Swahili Revised Union Version Akafunga siku arubaini mchana na usiku, mwishowe akaona njaa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa. Biblia Habari Njema - BHND Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa. BIBLIA KISWAHILI Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwishowe akaona njaa. |
Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arubaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.
Musa akaingia ndani ya lile wingu, akapanda mlimani; Musa akawa humo katika ule mlima siku arubaini, mchana na usiku.
Naye alikuwa huko pamoja na BWANA siku arubaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi.
kwa maana nilikuwa na njaa, mkanipa chakula; nilikuwa na kiu, mkaninywesha; nilikuwa mgeni, mkanikaribisha;
Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.
Mimi niwaiwanulia nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.
Nikaanguka chini mbele za BWANA siku arubaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote mliyofanya, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, kwa kumkasirisha.
Ndipo nikaanguka chini mbele za BWANA siku zile arubaini usiku na mchana nilizokuwa nimeanguka chini; kwa kuwa BWANA alisema atawaangamiza.
Na hapo nilipokwea mlimani kwenda kuzipokea mbao za mawe, nazo ni mbao za agano BWANA alilofanya nanyi, ndipo nikakaa mle mlimani siku arubaini usiku na mchana; sikula chakula wala kunywa maji.