Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
Mathayo 4:19 - Swahili Revised Union Version Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya nyinyi wavuvi wa watu.” Biblia Habari Njema - BHND Basi, akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya nyinyi wavuvi wa watu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya nyinyi wavuvi wa watu.” Neno: Bibilia Takatifu Isa akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” Neno: Maandiko Matakatifu Isa akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” BIBLIA KISWAHILI Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. |
Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, nenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.
Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.
Na alipokuwa akipita, akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata.
Baada ya hayo akatoka, akaona mtoza ushuru, jina lake Lawi, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate.
Akamwambia mwingine, Nifuate. Akasema, Bwana, nipe ruhusa kwanza niende nikamzike baba yangu.
Kesho yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate.
Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Yesu akamwambia, Ikiwa nataka huyu akae hata nitakapokuja, imekuhusuje wewe? Wewe unifuate mimi.