Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena.
Mathayo 4:11 - Swahili Revised Union Version Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo ibilisi akamwacha, nao malaika wakaja na kumhudumia. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo ibilisi akamwacha, nao malaika wakaja na kumhudumia. BIBLIA KISWAHILI Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia. |
Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena.
Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
Akawako huko jangwani siku arubaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwituni, na malaika walikuwa wakimhudumia.
Kila siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono, lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza.
Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana anakuja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulikana kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu malaika wote wa Mungu.