Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu.
Mathayo 27:52 - Swahili Revised Union Version makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema makaburi yakafunguka na watu wengi wa Mungu waliokufa wakafufuliwa; Biblia Habari Njema - BHND makaburi yakafunguka na watu wengi wa Mungu waliokufa wakafufuliwa; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza makaburi yakafunguka na watu wengi wa Mungu waliokufa wakafufuliwa; Neno: Bibilia Takatifu Makaburi yakafunguka na miili ya watakatifu waliokuwa wamekufa ikafufuliwa. Neno: Maandiko Matakatifu Makaburi yakafunguka na miili ya watakatifu waliokuwa wamekufa ikafufuliwa. BIBLIA KISWAHILI makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; |
Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu.
Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo.
Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.
Tena, wengi wa hao wanaolala katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.
Nitawakomboa kwa nguvu za kaburi; nitawaokoa kutoka kwa mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Huruma itafichika machoni mwangu.
Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha.
Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona kitendo cha kuuawa kwake kuwa sawa.
Maana, ikiwa tunaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.