Tamko alilolitamka BWANA katika habari zake ndilo hili, Bikira, binti Sayuni, amekudharau, na kukudhihaki sana; binti Yerusalemu ametikisa kichwa chake juu yako.
Mathayo 27:39 - Swahili Revised Union Version Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisatikisa vichwa vyao, wakisema, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana wakitikisa vichwa vyao na kusema, Biblia Habari Njema - BHND Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana wakitikisa vichwa vyao na kusema, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana wakitikisa vichwa vyao na kusema, Neno: Bibilia Takatifu Watu waliokuwa wakipita njiani wakamtukana huku wakitikisa vichwa vyao, Neno: Maandiko Matakatifu Watu waliokuwa wakipita njiani wakamtukana huku wakitikisa vichwa vyao BIBLIA KISWAHILI Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisatikisa vichwa vyao, wakisema, |
Tamko alilolitamka BWANA katika habari zake ndilo hili, Bikira, binti Sayuni, amekudharau, na kukudhihaki sana; binti Yerusalemu ametikisa kichwa chake juu yako.
Mimi nami ningeweza kunena kama ninyi; Kama roho zenu zingekuwa mahali pa roho yangu, Ningeweza kutunga maneno juu yenu, Na kuwatikisia ninyi kichwa changu.
Kwa maana vinywa viovu na vyenye hila vimefumbuliwa juu yangu, Vikinisema kwa ulimi wa uongo, Wamesema nami kwa ulimi wa uongo.
Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.
Je! Si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia, Angalieni, mtazame Kama kuna majonzi yoyote mfano wa majonzi yangu, Niliyotendwa mimi, Ambayo BWANA amenihuzunisha kwa hayo Siku ya hasira yake iwakayo.
Wakati uo huo wanyang'anyi wawili wakasulubiwa pamoja naye, mmoja katika mkono wake wa kulia, na mmoja katika mkono wake wa kushoto.