Akasema, Wavivu ninyi; wavivu; kwa ajili hii mwasema, Tupe ruhusa twende kumtolea BWANA dhabihu.
Mathayo 26:8 - Swahili Revised Union Version Wanafunzi wake walipoona, wakakasirika, wakasema, Ni wa nini upotevu huu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Ya nini hasara hii? Biblia Habari Njema - BHND Wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Ya nini hasara hii? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Ya nini hasara hii? Neno: Bibilia Takatifu Lakini wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Upotevu huu wote ni wa nini? Neno: Maandiko Matakatifu Lakini wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Upotevu huu wote ni wa nini? BIBLIA KISWAHILI Wanafunzi wake walipoona, wakakasirika, wakasema, Ni wa nini upotevu huu? |
Akasema, Wavivu ninyi; wavivu; kwa ajili hii mwasema, Tupe ruhusa twende kumtolea BWANA dhabihu.
Tena nikagundua kuwa juhudi zote, na ustadi wote katika kazi, hutokana na mtu kumwonea mwingine wivu. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.
mkisema, Mwezi mpya utaondoka lini, tupate kuuza nafaka? Na sabato nayo, tupate kuandaa ngano? Mkiipunguza efa na kuiongeza shekeli, mkidanganya watu kwa mizani ya udanganyifu;
Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! Nanyi mmelidharau, asema BWANA wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema BWANA.
mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya thamani kubwa alimkaribia akaimimina kichwani pake alipoketi chakulani.
Palikuwa na watu waliochukizwa katika nafsi zao wakisema, Kwa nini kupoteza marhamu namna hii?