Mathayo 26:70 - Swahili Revised Union Version Akakana mbele ya wote, akisema, Sijui usemalo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Petro akakana mbele ya wote akisema, “Sijui hata unasema nini.” Biblia Habari Njema - BHND Petro akakana mbele ya wote akisema, “Sijui hata unasema nini.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Petro akakana mbele ya wote akisema, “Sijui hata unasema nini.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui hilo usemalo.” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui hilo usemalo.” BIBLIA KISWAHILI Akakana mbele ya wote, akisema, Sijui usemalo. |
Tena ni nani uliyemwogopa na kumhofu, hata ukasema uongo, wala hukunikumbuka mimi, wala kuweka hayo moyoni? Je! Mimi sikunyamaza tangu zamani, hata huniogopi?
Na tazama, mmoja wa wale waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.
Lakini haya yote yamekuwa, ili maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.
Na Petro akamfuata kwa mbali mpaka behewa ya Kuhani Mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.
Na Petro alikuwa ameketi nje uani; kijakazi mmoja akamwendea, akasema, Wewe nawe ulikuwapo pamoja na Yesu wa Galilaya.
Naye alipotoka nje hadi ukumbini, mwanamke mwingine alimwona, akawaambia watu waliokuwako huko, Huyu alikuwapo pamoja na Yesu Mnazareti.
Vema. Yalikatwa kwa kutoamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope.
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.