Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii.
Mathayo 22:40 - Swahili Revised Union Version Katika amri hizi mbili hutegemea Torati yote na vitabu vya Manabii. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sheria yote ya Mose na mafundisho ya manabii vinategemea amri hizi mbili.” Biblia Habari Njema - BHND Sheria yote ya Mose na mafundisho ya manabii vinategemea amri hizi mbili.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sheria yote ya Mose na mafundisho ya manabii vinategemea amri hizi mbili.” Neno: Bibilia Takatifu Amri hizi mbili ndizo msingi wa Torati na Manabii.” Neno: Maandiko Matakatifu Amri hizi mbili ndizo msingi wa Torati na Manabii.” BIBLIA KISWAHILI Katika amri hizi mbili hutegemea Torati yote na vitabu vya Manabii. |
Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii.
Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yoyote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
Lakini lengo la agizo hili ni kuleta upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.
Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.