Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake.
Mathayo 22:30 - Swahili Revised Union Version Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana wafu watakapofufuka hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika mbinguni. Biblia Habari Njema - BHND Maana wafu watakapofufuka hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika mbinguni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana wafu watakapofufuka hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika mbinguni. Neno: Bibilia Takatifu Wakati wa ufufuo, watu hawataoa wala kuolewa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati wa ufufuo, watu hawataoa wala kuolewa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni. |
Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake.
BWANA wa majeshi asema hivi, Ikiwa utaenda katika njia zangu, na kushika maagizo yangu, basi utaihukumu nyumba yangu, na kuzilinda nyua zangu, nami nitakupa haki ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.
Ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie.
Angalieni msidharau mmojawapo wa wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni. [
Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hadi siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.
Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mtumishi mwenzako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.