Mathayo 22:23 - Swahili Revised Union Version Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku hiyo, baadhi ya Masadukayo wasemao wafu hawafufuki walimwendea Yesu. Biblia Habari Njema - BHND Siku hiyo, baadhi ya Masadukayo wasemao wafu hawafufuki walimwendea Yesu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku hiyo, baadhi ya Masadukayo wasemao wafu hawafufuki walimwendea Yesu. Neno: Bibilia Takatifu Siku hiyo hiyo Masadukayo, wale wasemao kuwa hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Isa na kumuuliza swali, wakisema, Neno: Maandiko Matakatifu Siku hiyo hiyo Masadukayo, wale wasemao kwamba hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Isa na kumuuliza swali, wakisema, BIBLIA KISWAHILI Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza, |
Na alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazawa wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?
Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na walinzi wa hekalu na Masadukayo wakawatokea,
Akaondoka Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo), wamejaa wivu,
waliopotoka kutoka kwenye kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha tokea, hata kuipindua imani ya watu kadhaa.