Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,
Mathayo 22:15 - Swahili Revised Union Version Ndipo Mafarisayo wakaenda zao, wakafanya shauri, jinsi ya kumtega kwa maneno. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha, Mafarisayo wakaenda zao, wakashauriana jinsi ya kumnasa Yesu kwa maneno yake. Biblia Habari Njema - BHND Kisha, Mafarisayo wakaenda zao, wakashauriana jinsi ya kumnasa Yesu kwa maneno yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha, Mafarisayo wakaenda zao, wakashauriana jinsi ya kumnasa Yesu kwa maneno yake. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Mafarisayo wakatoka nje wakaandaa mpango wa kumtega Isa katika maneno yake. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Mafarisayo wakatoka nje wakaandaa mpango wa kumtega Isa katika maneno yake. BIBLIA KISWAHILI Ndipo Mafarisayo wakaenda zao, wakafanya shauri, jinsi ya kumtega kwa maneno. |
Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,
Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo, Moyo wake hujikusanyia maovu, Naye atokapo nje huyanena.
Wameweka wavu ili kuninasa miguu; Nimevunjika moyo; Wamechimba shimo njiani mwangu; Lakini wao wenyewe wametumbukia humo!
Kwa maana wanaiotea nafsi yangu; Wenye nguvu wamepanga kunishambulia; Ee BWANA, si kwa kosa langu, Wala si kwa hatia yangu.
hao wamfanyao mtu kuwa amekosa katika neno, na kumtegea mtego yeye aonyaye langoni, na kumgeuza mwenye haki kwa kitu kisichofaa.
Hapo ndipo waliposema, Njooni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njooni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.
Maana nimesikia shutuma za watu wengi; hofu ziko pande zote. Rafiki zangu wote, wanaonivizia nisite, husema, Mshitaki, nasi tutamshitaki, huenda akahadaika, nasi tutamshinda, tutajilipiza kisasi kwake.
Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.
Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili upinzani mkuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.