na Yehoyakimu, mfalme, na mashujaa wake wote, na wakuu wake wote, waliposikia maneno yake, mfalme akataka kumwua; lakini Uria alipopata habari, aliogopa, akakimbia akaenda Misri.
Mathayo 14:5 - Swahili Revised Union Version Naye alipotaka kumwua, aliwaogopa watu, maana walimwona Yohana kuwa nabii. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Herode alitaka kumuua Yohane, lakini aliogopa watu kwa sababu kwao Yohane alikuwa nabii. Biblia Habari Njema - BHND Herode alitaka kumuua Yohane, lakini aliogopa watu kwa sababu kwao Yohane alikuwa nabii. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Herode alitaka kumuua Yohane, lakini aliogopa watu kwa sababu kwao Yohane alikuwa nabii. Neno: Bibilia Takatifu Herode alitaka sana kumuua Yahya, lakini akaogopa watu, kwa maana walimtambua kuwa ni nabii. Neno: Maandiko Matakatifu Herode alitaka sana kumuua Yahya, lakini akaogopa watu, kwa maana walimtambua kuwa ni nabii. BIBLIA KISWAHILI Naye alipotaka kumwua, aliwaogopa watu, maana walimwona Yohana kuwa nabii. |
na Yehoyakimu, mfalme, na mashujaa wake wote, na wakuu wake wote, waliposikia maneno yake, mfalme akataka kumwua; lakini Uria alipopata habari, aliogopa, akakimbia akaenda Misri.
Na tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, twaogopa mkutano; maana watu wote wamwona Yohana kuwa ni nabii.
Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.
Na tukisema ulitoka kwa wanadamu, watu wote watatupiga kwa mawe, kwa kuwa wamemkubali Yohana kuwa ni nabii.
Nao walipokwisha kuwatisha tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu; kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka;
Ndipo yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawapiga kwa mawe.