Mathayo 1:25 - Swahili Revised Union Version asimjue kamwe hadi alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini hakulala naye hata Maria alipojifungua mtoto wa kiume. Naye Yosefu akampa jina Yesu. Biblia Habari Njema - BHND Lakini hakulala naye hata Maria alipojifungua mtoto wa kiume. Naye Yosefu akampa jina Yesu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini hakulala naye hata Maria alipojifungua mtoto wa kiume. Naye Yosefu akampa jina Yesu. Neno: Bibilia Takatifu Lakini hawakukutana kimwili hadi Mariamu alipojifungua mwanawe; akamwita jina Isa. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini hawakukutana kimwili mpaka Mariamu alipojifungua mwanawe kifungua mimba, akamwita Jina lake Isa. BIBLIA KISWAHILI asimjue kamwe hadi alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU. |
Naye msichana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; lakini mfalme hakumjua.
Nitakasie mimi wazaliwa wa kwanza wote, kila afunguaye tumbo katika wana wa Israeli, wa binadamu na wa mnyama; ni wangu huyo.
Usikawie kuleta malimbuko ya matunda yako na ya vinywaji vyako. Mzaliwa wa kwanza katika wanao wanaume utanipa mimi.
Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.
Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;
Hata zilipotumia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.
akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.